Wednesday, 7 June 2017

Kanisa lafanya Ibada maalum kumshukuru Mungu Chelsea kutwaa EPL

Kanisa la Living Streams International lililopo Accra Ghana limeandaa na kufanya Ibada maalum kumshukuru Mungu kwa kuisaidia Chelsea F.C kumaliza vizuri msimu wa 2016/17 na kuibuka mabingwa wa Premier League.
Mchungaji wa Kanisa hilo ambaye ni shabiki mkubwa wa Chelsea aliwahamasisha waumuni wake kuvalia jezi za timu hiyo katika Ibada hiyo ambapo iliandaliwa keki maalum huku waumini wakiimba wimbo wa timu “Blue is the Colour”.
Mbali na hilo waumini wengine ambao sio mashabiki wa Chelsea waliruhusiwa kuvaa jezi za timu zao ambapo Mchungaji Mkuu ambaye ni shabiki wa Arsenal alialikwa kushiriki kwenye Ibada akiwaambia waumini lengo ni kutumia nguvu za soka kuzungumzia kuhusu Mungu.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search