Tuesday, 20 June 2017

Mkuu wa Wilaya ya Ubungo aagiza Waziri Mkuu mstaafu Sumaye akamatwe na polisi popote alipo
Naangalia hapa AZAM TV,Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mh Kisare Makori,anasema ameamua kumkamata Meya wa Halmashauri ya Ubungo na kuagiza Polisi wamuweke ndani sababu amekiuka taratibu za kazi kwa kuwaleta wanachama wa CHADEMA wa kanda ya Pwani na kuwatembeza katika miradi ya maendeleo ya halmashauri.

Mkuu huyo wa Wilaya ya Ubungo,anasema kwa sheria na taratibu,wenye mamlaka ya kukagua miradi ya maendeleo ni wajumbe wa kamati ya Maendeleo wa Halmashauri chini ya Meya/Mwenyekiti wa Halmashauri.Hivyo kitendo cha Meya kutembelea miradi ya maendeleo bila madiwani wa kamati husika ni kuvunja sheria,na dawa yake ni kukaa ndani na kufunguliwa mashtaka.

Ameagiza Sumaye na viongozi wengine wa CHADEMA kanda ya Pwani walioambatana na Meya,nao wasakwe na jeshi la Polisi na kutiwa ndani popote pale walipo,ili waweze kujibu ni kwanini walikuja kutembelea miradi ya maendeleo bila idhini ya mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ubungo.

Mkuu wa Wilaya anasema kitendo cha Meya kutumia ukumbi na majengo ya halmashauri kukutana na viongozi wa CHADEMA ni kinyume na kanuni na sheria za utumishi wa umma,hivyo ameagiza Meya huyo kukaa ndani kwa masaa 48 kabla ya kufunguliwa mashtaka,huku akisisitiza Sumaye na viongozi wengine wasakwe.
SOURCE:JAMII FORUM

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search