Wednesday, 7 June 2017

MOURINHO-NIPENI MORATA NA PESA NIWAPE DE GEA


Mvutano kati ya Manchester United na Real Madrid kuhusu David De Gea umeanza upya, ambapo Madrid wanamtaka De Gea kwa nguvu zote huku United hawako tayari kumruhusu De Gea aondoke United.

Taarifa zinaeleza kuwa wiki iliyopita klabu ya Manchester United iliitolea nje ofa ya Real Madrid ya thamani ya zaidi ya £50m na kuwataka Madrid waende wakajipange zaidi.

Kufuatia kasi kubwa ya Madrid ya kumtaka mlinda mlango huyo, Meneja wa Man United, Jose Mourinho kwa kuwa wana kipa mwingine mzuri, Sergio Romero, ameamua kuwapa Real Madrid ofa ili wampate David De Gea huku akiwapa masharti.

Mourinho amewataka Real Madrid kutoa kiasi cha £22m pamoja na mchezaji Alvaro Morata ili kumruhusu De Gea ajiunge Real Madrid.

Mourinho amesema kama Real Madrid watatoa kiasi hicho cha pesa pamoja na Morata ambaye hapewi sana namba katika kikosi cha Madrid, atakuwa tayari kumuacha De Gea aondoke

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search