Monday, 19 June 2017

NIMEAMUA KUMUACHA MPENZI WANGU SABABU YA SIMU

NAMWACHA Mchumba Wangu Kwa Sababu ya Simu
Nimegundua wanawake sio viumbe wazuri hata kidogo,nina umri wa miaka 36 na mchumba wangu ana umri wa miaka 34,tumekutana miezi minne iliyopita na uhusiano wetu ulikuwa mzuri kwani nilimwamini na kwa kweli ana uwezo kunizidi,mtakumbuka miezi ya hapo nyuma nilileta mada hii hapa,ilikuwa ni true story kabisa

Kitu kimoja ambacho huyu dada amekuwa akinisumbua nacho ni simu zake mbili za mkononi,huko nyumba tumewahi kugombana mara kadhaa kwa ajili ya simu,yaani anazificha na hataki kabisa mimi nizishike japokuwa kila simu ina password

Jana usiku nililala kwake lakini asubuhi nilipoamka nikagundua simu zake hazipo hapo chumbani kwake,nikamuuliza simu zako ziko wapi?

Akachukua begi lake la mkononi na ku search ndani yake hakuna kitu,halafu akawa kama ameshtuka na kusema nilizisahau kwenye gari jana jioni,nikachukua fungua za gari na kwenda kuzichukua lakini sikuona kitu

Nilipomuuliza zaidi akawa mkali na kuniwakia eti simwamini kwa sababu ya simu,kilichonishangaza ni kwa nini awe mkali kuulizwa habari ya simu??niliamua kuondoka asubuhi ile ilikuwa saa kumi na moja na kuchapa yeboyebo zangu kurudi kwangu

Nimeamua kumwacha kwa sababu japo nilishaanza kumwamini lakini trust yangu imeuwawa na kitendo cha yeye kuficha sana simu

kwani hizo simu zina nini cha siri??nilikuwa nataka tufunge ndoa kabisa mwaka huu lakini kwa mpango huo nitakaa alone milele hapa duniani

Bora niishi peke yangu kuliko kuwa na mwanamke mwenye siri
this is true story!!!!

By Lameck

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search