Tuesday, 20 June 2017

NISHA ADAIWA KUTOKA NA BWANA WA SHILOLE

STAA wa filamu za Kibongo, Salma Jabu ‘Nisha’ anadaiwa kuwa kwenye mahaba motomoto na aliyekuwa mpenzi wa msanii mwenzake, Zuwena Mohammed ‘Shilole’ anayejulikana kwa jina la Boy Caro. Chanzo makini kililieleza Risasi Jumamosi kuwa, Nisha anapika na kupakua na mwanaume huyo bila hata aibu ambapo amehama Mbezi Makonde jijini Dar alikokuwa akiishi mwanzo na kuhamia Mikocheni kwa mwanaume huyo.


“Mapenzi ya Nisha na Boy Caro siyo siri tena kwani wanaishi pamoja, wanapika na kupakua hata hivi karibuni aliweka mtandaoni picha ya mkono wa mwanaume uliochorwa tatuu ambapo watu waligundua kuwa ni wa Boy Caro kwani aliichora wakati yupo na Shilole.


“Kiukweli wasanii tumekuwa tukijidhalilisha sana na tunamshangaa Nisha kula makombo ya mwenzake Shilole, je likija suala la ugonjwa si ndiyo tutakufa wote jamani? Maana wasanii wa kike tumezidi sana kushea mabwana,” kilimwagika chanzo ambacho ni msanii wa filamu ambaye hakutaka kuchorwa jina lake gazetini.

Baada ya kupata ubuyu huo wa moto, mwandishi wetu alimtafuta Nisha ili kujua ukweli wa madai hayo, alipopatikana alisema;“Jamani kwani kuwa karibu na Boy Caro ni tatizo? Kama ni Shilole walishaachana, ukaribu unaweza usiwe wa mapenzi, unaweza kuwa wa kikazi na mambo mengine, kuhamia Mikocheni siyo kwa ajili yake bali niliamua kubadilisha mazingira tu.”

SHILOLE ANASEMAJE? “Huyo mtu nilishaachana naye na sikuwahi kumpenda labda yeye ndiye alinipenda sana ndiyo maana hata nilipomuacha alichanganyikiwa, sijawahi kujuta kumuacha hivyo kama yupo na huyo hayanihusu mimi, bidii yangu ni kwenye kazi tu kwa sasa.”

STORI: GLADNESS MALLYA

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search