Thursday, 1 June 2017

RAIS MAGUFULI AFANYA UTEUZI WA MAGAVANA WAWILI WA BENKI KUU


Rais John Magufuli jana, Jumatano ameteua manaibu Gavana wawili wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

Taarifa ya Ikulu imesema, Rais amemteua, Dk Yamungu Kayandabila kuwa Naibu Gavana anayeshughulikia Uchumi na Fedha na Dk Bernard Yohana Kibese (Uthibiti na Usimamizi wa Sekta ya Fedha).

Kabla ya uteuzi huo, Dk Kayandabila ambaye anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Dk Natu Mwamba aliyememaliza muda wake, alikuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi,  Nyumba na Maendeleo ya Makazi.

 Dk Kibese aliyekuwa mtaalamu wa uchumi na fedha wa BoT, anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Lila Mkila ambaye amemaliza muda wake.


index.jpeg

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search