Tuesday, 20 June 2017

Sumaye: Serikali itambue CHADEMA ipo kisheria, wasitake vurugu bila sababu

Image result for SUMAYE
Sumaye ameiomba Serikali iache kuwafanyia fujo CHADEMA. wanayo haki ya kutembelea Sehemu walizoshinda ili kuona kama kweli Madiwani wao wanafanya kazi walizowaahidi wananchi. 

Hapa Ubungo kuna diwani wa CHADEMA, sisi kama Viongozi wake tumekuja kuona utendaji wake je anafanya kazi kweli au hafanyi. Sasa kosa lipo wapi? 

Polepole na Bulembo wa CCM wanazunguka kila Halmashauri nchi wala hawakatazwi na haiwi nongwa. Lakini chadema wakitembelea pale wanapoongozwa wanakamatwa wanatiwa ndani. 

Tunaomba Serikali ituache tuwatumikie wale waliotuchagua sababu hii miradi tunayoitembelea sio ya Chadema tu bali itatumiwa na Vyama vyote. 

"Tunaomba tu Serikali ituvumilie, CHADEMA ni chama halali kisheria na kinafanya kazi yake yake kwa mujibu wa sheria na Katiba ya nchi" Mjumbe Kamati Kuu CHADEMA na Waziri Mkuu mstaafu, Mhe. Frederick Sumaye.

MY TAKE:

Mjusi ukimkimbiza sana akifika ukingoni ambapo mbele hakuna njia tena, hugeuka nyoka na kuanza kukukimbiza wewe. Siasa CCM wanazofanya hazijawahi kufanikiwa sehemu yoyote Duniani. Kwamba mshindani wako unamfunga mikono kwa nyuma halafu unataka mpande ulingoni kupambana kisha unajisifu umeshinda. Ni kutojitambua na ni aibu.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search