Monday, 5 June 2017

Wabunge Ester Bulaya na Halima Mdee Wafungiwa Vikao vya Bunge kwa mwaka mzima

  1. pic+mdee+out.jpg
  Halima Mdee na Esther Bulaya

  Hukumu ya Halima Mdee na Esther Bulaya zinasomwa sasa. Sijui kama watapona.

  Dodoma. Halima Mdee na Esther Bulaya wamehukumiwa kutohudhuria vikao vyote vya bunge linaloendelea mpaka mkutano ujao wa Bunge la Bajeti ya 2018/19.

  Hukumu hiyo imeungwa mkono na wabunge wengi waliopitisha azimio hilo.

  Mapema leo, Jumatatu Kamati ya Maadili ilisema Bulaya na Mdee wamemaliza adhabu za kawaida zilizopo kwenye kanuni za bunge.

  Hata hivyo, Bunge liliendelea kujadili makosa ya wabunge hao wa Bunda na Kawe.

  Mwenyekiti wa kamati hiyo, George Mkuchika aliliomba Bunge kujadili adhabu inayostahili kulingana na makosa yao.

  Kanuni inasema, mbunge anayefanya kosa la kwanza anaweza akazuiwa kuhudhuria vikao visivyozidi 10 na atayakosea kwa mara ya pili anaweza kuzuiwa kuhudhuria vikao visivyozidi 20.

  UPDATES:

  => Shauri linayowahusu Esther Bulaya Mbunge na Halima Mdee Mbunge la kudharau Mamlaka ya Spika kinyume na kifungu cha 26 d chaa sheria ya kinga madaraka na haki za bunge.

  => Katika kikao cha mkutano wa saba wa bunge la 11 kilichofanyika tarehe 2 mwezi juni, kwa Mamlaka uliyo nayo chini ya kifungu cha 74 a & b, ya kanuni za kudumu za bunge, ulimtaja Mheshimiwa Esther Bulaya kwamba amedharau mamlaka ya Spika na Uliagiza yeye na Halima Mdee wafike mbele ya Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kujibu tuhuma hizo za kudharau Mamlaka ya Spika.

  => Chanzo cha Shauri: Katika kikao cha 40 kilichofanyika tarehe 2 juni 2017 lililokuwa linajadili Makadilio ya matumizi na mapato ya Wizara ya nishati na Madini kwa mwaka 2017/2018, wakati kikao hicho kinaendelea, Mheshimiwa Livingstone Joseph Lusinde(mb) alipewa nafasi ya kuchangia katika mjadala huo, Wakati akiendelea na Mjadala wake, Mheshimiwa John John Mnyika (MB) alisimama kuomba taarifa kuhusu utaratibu naye aliruhusiwa na Mheshimiwa Spika. Baada ya kutoa taarifa yake, Mheshimiwa Lusinde aliruhusiwa kuendelea kuchangia, kabla hajaendelea na kutoa mchango wake, Mbunge John Mnyia alisimama tena bila kufuata taratibu za Bunge na kuanza kusema bila ruhusa ya Spika, akidai kuwa kuna Mbunge amemuita kuwa yeye ni Mwizi.

  => Mheshimiwa Spika alimtaka Mnyika akae chini ili mjadala uendelee. Hata hivyo Mbunge huyo aliendelea kuzungumza bila idhini ya spika na Mheshimiwa Spika alimuamru Mpambe wa Bunge (sergeant at army) amtoe Mnyika nje ya Ukumbi wa Bunge. Na kwamba kutokana na utovu wa nidhamu asihudhurie bunge hadi tarehe 9june mwaka huu.

  => Wakati Mpambe wa bunge akimtoa Mnyika katika ukumbi wa Bunge, Halima Mdee alionekana akiwakimbilia Askari hao na kuvuta mashati na makoti yao ya Askari wawili kati yao waliokuwa wanamtoa nje Mnyika. Huku Esther Bulaya alionekana akisimama na kuanza kuzungumza bila idhini ya bunge na kutangatanga huku na huku akiwahimiza wabunge wa kambi ya Upinzani kutoka nje ya Ukumbi. Mheshimiwa Spika alimuonya Bulaya lakini aliendelea kufanya vitendo hivyo. Mheshimiwa BUlaya na Wabunge wote wa Upinzani walitoka nje isipokuwa mbunge mmoja.

  => Juliana Shonza wakati akichangia amesema Wabunge hawa wamekuwa na Mazoe mabaya ya kudhalau bunge ukizingatia ni Wabunge wazoefu waliotakiwa wawe wa Mfano. Anataka Wazuiliwe Vikao vyote vya bunge. Vikao vyote vilivyobakivya mkutano wa Saba, nane na Vikao vyote vya tisa.

  Spika awapongeza kamati ya Maadili kwa kazi walioifanya Wakati wa Wikendi na Wabunge kwa jinsi Walivyopokea na Kujadili Nawashukuruni sana.

  => "Ndugu zangu hawa Wabunge watatu ambao tumeshughulika nao kuanzia juzi, ni wabunge wazoefu kama mlivyosema, na sisi tumekuwa nao katika uongozi hapa kwa bunge lililopita na hili, Mimi nikiwa Naibu spika Mama Makinda akiwa Spika, tumetumia muda Mwingi tukisema jamani jamani, wote waliokuwepo ni Mashahidikwa jinsi ambavyo tulivyojitahidi sana kwa hawa watu watatu.

  => Lakini hapa ndipo tulipofika kwamba sasa lazima hatu zianze kuchukuliwa. Yaani katika kufanya Hivi, Moyo wangu mweupe kabisa yaani hakuna tatizo. Kwa sababu inasitahili, yupo binadamu lazima umfike mahali ambapo apate lugha ambayo anaweza kuielewa sabau lugha nyingine hazieleweki".

  => "Kwa Mwendo huu kwa yule mwenye macho ambaye angependa kuona Vizuri mtaona Trend inavyoenda. Kwa Azimio hili manake mkutano huu wa Saba hawapo, Mkutano unaokuja wa Nane hawapo, Mkutano wa tisa Februali hawapo ina Maana Tutakutana Mkutano unaokuja wa Bajeti. Ameongeza Spika."

  => "Anayetaka kwenda popote pale na aende na maamuzi yoyote yale na yafanywe, itakua ndo mwanzo wa constitutional crisis katika nchi hii kama mimi ni Spika hapa. Tutarudi hapa na badala ya Adhabu ya Mwaka mmoja tutapiga tena miaka kadhaa, halafu tuone sasa kitakachotokea, hatuwezi kuvumilia kuona bunge hili likivurugwa kwa namna yoyote ile. Hatuwezi."

  => "Mheshimiwa Ally Salehe alisema, Kwamba yeye ndo alianzisha zoezi la kwenda nje kushauriana kwa ndugu zangu wa kambi ya Upinzani. Sina tatizo naye au yoyote katika hilo. ingawaje ni jambo kwenye kanuni halipo. Katika kushauriana kwao, wengine wakawa wanaropoka wanavyotaka, nichukue nafasi hii kuwapa onyo wachache, nafikiri nliwahi kusema kwamba Majengo haya ya Bunge yapo so secured kiasi ambacho hatukukosi na tuna ushahidi wa kutosha. Kwa watu ambao kwa Makusudi walikuwa wakinitukana mimi mwenyewe binafsi na kusema maneno ya hovyo sana katika bunge hili.

  => Kwenye hayo Mashauriano ya Ally Salehe na wenzake huko nje. Natoa onyo na Ushahidi tunao wa kutosha kwa Mheshimiwa Rhoda Kunchela kwa Matusi na dharau alizokuwa akizifanya, na niwambie ndugu zangu huu sio ubinadamu, hamuwezi kuunga mkono mambo kama haya na hatuwezi kwenda hivi. Hatuwezi kwenda hivi Ally Salehe hatuwezi kwenda hivi. Rafiki yangu Kubenea hatuwezi kwenda hivi.

  => Yapo mambo lazima tukubaliane hatuwezi kwenda hivi. Rhoda Kunchela umekuja juzi unanitukana Kweli!!..nimekukosea nini?. Suzan Kiwanga Unanitukana? anatukana bunge anawatukana ninyi? Mheshimiwa Katani Katani unatukana? Na hii Katani ni mara ya pili kwenye Vitabu vyangu rekodi za tabia mbaya zilizopitiliza."

  => "Tunalo tatizo, kuna wakati ndugu zangu wa Kambi za Upinzani kaeni jaribuni kuangalia baadhi ya mambo ya hovyo na muambiane, wekeni sawa. Hamuwezi kutengeneza genge la kutetea Maovu, ninyi mkawa kundi la kuwa kundi moja katika maovu, mbona katika Maovu Mungu mwenyewe hataki ndo maana kuna mwezi mtukufu. Yaani genge la maovu huwa halifaulu hata siku moja. Na ninyi ni watu wema, mna watu wazuri sana nawafahamu, najua wengi mnawiwa mnapata tabu mfanyeje, mnaenda kama kundi sasa tutafanyaje.

  => Lakini lazima mfike mahali muambiane wewe ukienda njia hii utaenda Peke yako, hatuwezi kwenda wote. Mimi naamini katika wema huu mimi nina imani na nyinyi na wabunge wana imani nan ninyi mtakaa, yale ambayo mnadhani kwamba tunahitaji na sisi kurekebika mtuambie lakini yale machafu lazima yarekebishwe,lazima na ninyi muwe na moyo wa kuambiana, hawa wenzenu wanaambiana kama hamjui.

  => Hawa wanaambiana, sio kwamba wote ni wazuri hivo, wanaambiana. Na ninyi mjenge utamaduni huo labda mnafanya hivyo basi ongezeni bidii." Amesema Spika

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search