Tuesday, 13 June 2017

WABUNGE WAJAZANA MGAHAWANI KUFUATILIA RIPOTI YA PILI YA MCHANGA

Bungeni

Wakati kipindi cha maswali na majibu kikiendelea bungeni leo Jumatatu, baadhi ya wawakilishi wametoka ukumbini na kwenda kantini ya Bunge kufuatilia ripoti ya pili ya usafirishaji wa mchanga wa dhahabu inayorushwa mubashara kupitia vituo vya televisheni kutoka Ikulu jijini Dar es Salaam.

Baadhi wa wabunge wakinywa chai huku wengine wakijiburudisha kwa vinywaji baridi wamekuwa kwenye makundi matatu kulingana na idadi ya runinga zilizopo katika kantini hiyo.

Ilipotajwa hoja ya udanganyifu katika taarifa inayotolewa kisha Rais John Magufuli na Waziri Mkuu wake, Kassim Majaliwa kuonekana kwenye kioo cha televisheni wakitazamana, wengi wameguna ishara kwamba hoja hiyo ni nzito.

 Hata yaliposomwa makosa ya jinai yanayoambatana na usafirishaji huo, miguno mingine imesikika.

 Ukwepaji kodi, udanganyifu na makosa mengine yaliyobainishwa na mwenyekiti wa kamati hiyo ya pili, yamewagusa wabunge wengi wanaofuatilia.

 Bila kujua kama wanaambizana au ni shauku ya kila mmoja kusikia kinachowasilishwa na kamati hiyo, idadi yao imekuwa ikiendelea kuongezeka kantini

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search