Tuesday, 11 July 2017

ALICHOKISEMA LADY JAYDEE BAADA YA PROFESA J KUFUNGA NDOA

Related image
Msanii wa Bongo, Lady Jaydee amempa pongezi za kutosha msanii mwenzie Professor Jay kwa uamuzi aliyofikia wa kufunga ndoa.

Weekend iliyopita siku ya Jumamosi Prof Jay alifunga ndoa na mchumba wake wa siku nyingi ‘Grace’ ambaye tayari walishajaliwa mtoto mmoja.

Kuhusu hilo Lady Jaydee amesema, “Kwanza nimpongeze Prof Jay kwa hatua aliyochukua, ni hatua nzuri katika maisha kwa sababu kwanza ni kuzaliwa, pili ni kuoa au kuolewa na ya tatu ni kufa, kwa hiyo hii ni harusi ya pili katika maisha yake nimpongeze sana kwa uamuzi alioufikia,” ameiambia Planet Bongo ya EA Radio na kuongeza. “Nimtakie kila la kheri katika maisha yake ya ndoa yenye furaha na mafanikio. Professor kama kaka yangu na kama rafiki yangu ni mambo mengi tumepitia pamoja, tumeweza kusapotiana katika kazi na mambo mengine, kwa hiyo ni furaha kwangu, si kama msanii mwenzake bali kama mwanafamilia,” ameeleza Lady Jaydee

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search