Wednesday, 12 July 2017

ALIYETOBOLEWA MACHO NA SCORPION ADAIWA KUMSHUSHIA KIPIGO MKEWE NA KUTELEKEZA FAMILIA NA KUHAMIA KWA MWANAMKE MWINGINE

Kumbukumbu zikiwa bado mbichi vichwani mwa watu juu ya tukio la kutobolewa macho kwa kijana Said Mrisho linalotajwa kufanywa na Salum Njwete ‘Scorpion’, mapya yameibuka yakiihusu familia hiyo kwa kile kinachoelezwa kuwa Said amemtekeleza mkewe na watoto.
Katika mahojiano Exclusive kupitia Global TV Online, mke wa Said, Stara Soud alisema kisanga hicho kinadaiwa kutokea hivi karibuni siku chache baada ya wawili hao kuhamia kwenye nyumba ya kupanga maeneo ya Majichumvi, wakitokea Mabibo-Hosteli Ubungo na likifuatiwa na varangati la aina yake ambapo soo hilo lilitinga polisi kabla ya kuamriwa kuhamia Ustawi wa Jamii.
“Baada ya kuhamia Majichumvi, siku hiyohiyo Said akaniambia anatarajia kusafiri usiku, hivyo nimuandalie nguo na mimi bila kusita wala kuwa na wasiwasi nilifanya kama alivyoniagiza, akaja akachukua nguo na kusema tena atalala kwa rafiki yake ili wadamke usiku, akaondoka lakini baadaye alinipigia simu na kuniuliza kama nilikuwa bado naweka vitu sawa na kunijulisha kuwa kuna mahali amekaa akipata chakula.
“Alipomaliza kuniambia hivyo, akadhani simu imekatika lakini bado ilikuwa hewani akawa anasema yaani huyu anadhani ninasafiri, nitamkimbia taratibu hadi tuachane kabisa, hakika niliumia na kuanza kulia kujua kumbe mume wangu ananifanyia uhuni wakati nina watoto wanne wengine wakiwa wachanga wa mwezi mmoja,” alisema Stara na kumalizia;
“Kuna nyumba ya zamani ambayo tulitaka kuhamia kabla ya huku Majichumvi na kuna baadhi nya vitu vyetu vilikuwa huko, nikampigia simu mama na hapohapo mimi na dada yangu tukaenda huko kubahatisha kama tutamkuta, kweli tulimkuta na alianza kufanya fujo akampiga mtoto na dada yangu, baadaye kesi ikahamia polisi, akiwa amenisingizia kwamba mimi na ndugu zangu tumemfanyia fujo na kumuibia shilingi milioni mbili, tukashauriana suala hilo lifike Ustawi wa Jamii ambapo kesho tutafanya hivyo,” alisema Stara.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search