Wednesday, 12 July 2017

ANGALIA VIDOE IKIONESHA EVERTON ILIVYOWASILI

Klabu ya Everton tayari imewasili Jijini Dar es Salam dakika chache zilizopita ikiwa inatokea nchini Uingereza huku ikiwakosa wachezaji wake watatu muhimu katika kikosi hicho kutokana na majeruhi waliyokuwa nayo.

Waziri mwenye dhamana ya Michezo Dk harrison Mwakyembe akisalimiana na Wayne Rooney.
Pamoja na hayo, timu ya Everton imeongozwa na mchezaji nyota Wayne Rooney pamoja na Davy Klaassen na Michael Keane ambao pia wamejiunga na klabu hivi karibuni.

Kikosi kamili cha Everton kilichotua leo ni Maarten Stekelenburg, Mateusz Hewelt, Chris Renshaw, Tom Davies, Phil Jagielka, Ashley Williams, Callum Connolly, Jonjoe Kenny, Michael Keane, Muhamed Besic, Leighton Baines, Morgan Schneiderlin, James McCarthy, Davy Klaassen.


Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search