Monday, 31 July 2017

DARAJA REFU ZAIDI DUNIANI LA KUPITA WATU JUU KABISA LAFUNGULIWA USWISI


Daraja lililotundikwa lenye mita 500 linalokisiwa kuwa refu zaidi duniani limefunguliwa katika mji wa Zermatt nchini Uswizi.
Daraja hilo lenye urefu wa mita 494 kwa jina Europabrucke limetundikwa mita 85 juu .
Bodi ya utalii ya Zermatt inasema kuwa ndio daraja refu zaidi duniani ,ijapokuwa daraja la mita 405 mjini Reutte Austria limetundikwa mita 110 juu kutoka ardhini.

Daraja hilo linachukua mahala pa daraja jingine ambalo lilikuwa limeharibiwa na mwamba.
Daraja hilo jipya ambalo lina uzito wa tani nane limewekwa kifaa cha ambacho kinalizuia kuyumbayumba ,kulingana na bodi ya watalii ya Zermatt.

Daraja hilo lipo kati ya Zermatt na Grachen kusini mwa Switzerland.
Chanzo-BBC

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search