Monday, 17 July 2017

FLORA :MWANAUME HAKURIDHISHI KINYUMBA WANINI KUENDELEA NAE

Akihojiwa na kituo cha redio Swahili FM leo asubuhi, Flora Mwenda (zamani Flora Mbasha) amefunguka mambo mazito sana. Huku akiwa live redioni, amemuambia mtangazaji wa kipindi kuwa moja ya sababu zilizopelekea kutengana na mume wake wa zamani, Emmanuel Mbasha, ni ugoigoi wake kitandani.
“Unajua mimi nimeokoka siwezi kutoka nje ya ndoa, mwanaume anapokuwa hakuridhishi kiunyumba hakuna haja ya kuendelea kubaki naye”, alisema Madam Flora. Mtangazaji alipombana afunguke zaidi, alikataa na kumueleza kwamba kila kitu amekisimulia kwenye kitabu chake kinachoitwa Siri Za Flora ambacho ameanza kukizambaza katika mikoa mbalimbali.
Mtakumbuka kwamba siku za nyuma kuna baadhi ya watu walimsingizia kutembea na Askofu Gwajima, tuhuma ambazo amezikanusha vikali kwenye kitabu chake. Sasa wale wote mliomtungia uongo Madam Flora mmeumbuka mchana kweupe.
Huyo ndiye Madam Flora Mwenda, The Born Again

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search