Monday, 10 July 2017

HALIMA MDEE AFIKISHWA MAHAKAMANI

Mbunge wa Jimbo la Kawe Halima Mdee amefikshwa katika mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu leo Jijini Dar es salaam.

Halima Mdee (Chadema), alikamatwa Julai 4 Jioni, na Jeshi la Polisi Mkoa wa Kinondoni kwa na agizo la Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi. Kwa kile kilichodaiwa alitoa lugha ya kumtukana Rais Magufuli.

Pichani ni Mbunge wa Jimbo la Kawe Halima mdee, akiwa amehifadhiwa katika ukumbi wa Wazi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akisubiri kusomewa kesi yake. 
Mbunge wa Jimbo la Kawe Halima mdee akisalimiana na Mbunge wa Bunda Mjini kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) , Ester Bulaya, akiwa amehifadhiwa katika ukumbi wa Wazi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akisubiri kusomewa kesi yake.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search