Thursday, 20 July 2017

MBUNGE WA JIMBO LA TEMEKE ABDALLAH MTOLEA AWEKWA NDANI

Mbunge wa Temeke, Abdallah Mtolea yuko rumande tangu jana baada ya kukamatwa na Polisi akituhumiwa kuendesha gari ambalo bima yake ilikuwa imeisha muda.

Akithibitisha kukamatwa kwake leo  Alhamis Julai 20, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, Gilles Mrosso amesema mbunge huyo yuko rumande tangu jana jioni.

Amesema amekamatwa na askari wa usalama barabarani Temeke akiendesha gari ambalo bima yake ilikuwa imeisha muda  wake.

“Askari wa usalama barabarani walipomhoji aliamua kuwapuuza na kuondoka zake,” amesema.

Amesema polisi walimfuatilia na kumkamata na sasa anaendelea kuhojiwa ili aweze kufikishwa mahakamani.

“Atafikishwa mahakamani kama tunavyofanya kwa raia yoyote, nafasi yake kama mbunge haiwezi kuwa sababu ya kutofuata sheria,” amesema.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search