Thursday, 6 July 2017

MBUNGE Waitara Ahojiwa Dodoma Kwa Futari Aliyoiandaa Dar


Dodoma. Mbunge wa Ukonga, Mwita Waitara amehojiwa na ofisa wa polisi katika viwanja vya Bunge kwa kile alichokieleza ni kutokana na futari aliyoiandaa jimboni kwake.

Mwita amesema mahojiano hayo yanatokana na futari ambayo alimwalika Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa, ambaye alitoa maneno yanayodaiwa  yalionyesha kuikera Serikali.

"Amejitambulisha kwangu kuwa ni polisi, lakini jana (Julai 4) pia nilipigiwa simu na ofisa upelelezi Mkoa wa Dodoma akinitaka niende kwa mahojiano," amesema Waitara.

Mahojiano kati ya Waitara na ofisa huyo yamefanyika eneo la mapokezi katika jengo la utawala la Bunge muda mchache baada ya mkutano wa saba wa Bunge kuahirishwa leo (Julai 5).

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search