Thursday, 6 July 2017

MKUU WA WILAYA YA ILEMELA AACHIA NGAZI


Mkuu wa Wilaya ya Ilemela , Dk Leonard Masale, ameachia ngazi baada ya kufikisha umri wa kustaafu.


Akithibitisha taarifa hizo mchana wa leo Julai 5, Dk Masala amesema hayuko ofisini tangu Julai Mosi baada ya kufikia umri wa miaka 60, ambao ni wa kustaafu kwa lazima kwa mtumishi wa umma.


Amesema hivi sasa nafasi yake inakaimiwa na Mkuu wa Wilaya ya Magu, Khadija Nyembo, na yeye tayari amepokea mafao yake ya kustaafu kutoka mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma, PSPF, baada ya kuwaandikia barua kuwajulisha kuhusiana na kustaafu kwake miezi sita iliyopita.Hata hivyo, kiongozi huyo amesema yuko tayari kulitumikia taifa katika nafasi yoyote atakayopewa iwapo atahitajika kwani hajachoka nabado ana uwezo wa kufanya kazi.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search