Thursday, 27 July 2017

MSIKILIZE LISSU AKIONGEA NA WAANDISHI WA HABARI BAADA YA KUTOKA MAHABUSU

 1. Baadaye ya kuachiwa kwa dhamana Mwanasheria wa Chadema Tundu Lissu muda huu anaongea na waandishi wa habari.
  ==>>Tundu Lissu "Hakuna gereza litakalotunyamazisha. Mwambieni Magufuli, tutanyamaza tukiwa wafu. Wafu huwa hawasemi"

  =>Tundu Lissu "wanataka tunyamaze ili waendeshe nchi hii wanavyotaka wao, Taifa hili ni la mfumo wa vyama vingi, tunayo haki ya kufanya mikutano, tunayo haki ya kufanya maandamano na tunayo haki ya kutoa maoni yetu. Kwa msingi huo hakuna wa kutunyamazisha, nchi hii siyo mali ya mtu binafsi.”

  =>Tundu Lissu "naomba niweke wazi kabisa. Hakuna gereza, wala mahabusu, wala polisi, wala usalama wa taifa, wala Magufuli na wala mtu yeyote atakayetunyamazisha. Narudia. “Hatutakubali kunyamazishwa. Kwa sababu, tukinyamaza kwa kuogopa mahabusu, tukaogopa magereza, tukaogopa mabomu ya mapolisi, tukanyamaza. Nchi hii, inaangamia.”

  =>Tundu Lissu "Hatutaogopa kunyamazishwa na mtu yeyote kwa sababu tukinyamaze nchi hii inaangamia"

  =>Tundu Lissu Njia rahisi ya kwenda mbinguni ni kupinga uonevu.
  "Mwambieni Magufuli tutanyamaza tukiwa Wafu"

  =>"Tundu Lissu Siku yoyote ukimatwa na Jeshi la Polisi na kuambiwa wanaenda kukupima mkojo waambie mimi sitaki kwa sababu Jeshi la Polisi hawana mamlaka hayo kisheria. Tundu Lissu
  CREDIT:JAMII FORUM 

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search