Thursday, 20 July 2017

PICHA :HIVI NDIVYO RAIS MAGUFULI ALIVYOMPOKEA NKURUNZINZA


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt John Pombe magufuli akiwa ameambatana na mgeni wake  Rais wa Burundi,Pierre Nkurunziza aliewasili mapema leo katka uwanja wa mpira wa Lemela mjini Ngara,Rais Dkt Magufuli amempokea Rais Nkurunziza akiwa kwenye ziara yake kikazi mkoani Kagera.
Aidha Rais Nkurunziza baada ya kupokelewa na Mwenyeji wake Rais Dkt Magufuli,alipata wasaa wa kuwasalimia wananchi mbalimbali waliofika kumpokea katika uwanja huo wa mpira mjini Ngara.

Rais wa Burundi Pierre Nkurunzinza leo July 20, 2017 amewasili Tanzania katika Wilaya ya Ngara, Kagera na kupokelewa na mwenyeji wake Rais Magufuli na kupigiwa mizinga 21 pamoja na kukagua gwaride lililoandaliwa na JWTZ.
Baada ya mapokezi hayo msafara wa viongozi hao ulielekea Ngara Mjini ambako watafanya mazungumzo mafupi kabla ya Rais Magufuli kuwahutubia wakazi wa Ngara katika Mkutano wa hadhara utakaofanyika viwanja vya Posta.
FULL VIDEO: Mapokezi ya Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza aliyewasili Tanzania na kupokelewa na Rais Magufuli leo…PLAY kwenye hii VIDEO kutazama kila kitu!!!!

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search