Monday, 17 July 2017

RAMMY GALIS NAJUTA KUWA KWENYE MAHUSIANO NA MASOGANGE

Muigizaji wa kiume anaefanya vizuri katika tasnia ya Bongo Movie Tanzania, Rammy Galis amefunguka kilichomuondoa kwa aliyekuwa mpenzi wake Agnes Masogange .
Rammy amesema kuwa Agnes Masogange alikuwa na mapungufu mengi ambayo hakuweza kuyavumilia katika mahusiano yao ya kimapenzi .
“Kila binadamu ana mapungufu yake siwezi kusema nimekamilika au yeye hakuwa perfect. Mimi nina mapungufu yangu na agnes ana mapungufu yake lakini mapungufu yanapozidi upande mmoja ndipo mtu unapochukua maamuzi haraka kwahiyo mimi ninaweza kusema mapungufu yake yalikuwa yamezidi kuliko yangu mimi katika mahusiano yetu hivyo sikuona budi kuendelea na maisha yangu” alisema Rammy .
“Nimepoteza tu muda, unajua unapokuwa katika mahusiano unakuwa haujui kama kuna kitu una’loose zaidi ya kujiona wewe una’gain kwasababu ni mapenzi yanakusukuma kwenye moyo wako kwamba bado unahitajika kuwepo na bila kujua siku ambayo mtaachana utakuja kugundua kwamba umepoteza muda mwingi kwahiyo majuto yangu ni muda tu ambao nimepoteza kwa Agnes hivyo vingine havielezeki kwenye media” aliongeza rammy .
Mkali huyo anaefanya vizuri katika tasnia ya Bongo Movie amesema hakuna msichana wa kibongo anaemfikiria kutoka nae kimapenzi kwasababu tiyari ana mtu mwingine ambaye yupo bara la America .
Kipindi cha mapenzi yao @rammygalisofficial na @officialagness2 walicheza Movie ambayo wameipa jina la ‘The Secret Job’ inayotarajiwa kutoka hivi karibuni ambapo movie hiyo amedai kuwa inaelezea zaidi mahusiamo yao

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search