Friday, 7 July 2017

SERIKALI YA UGANDA YAPIGA MARUFUKU KUJIPODOA NA KUFUGA KUCHA

Kama ulikuwa una ndoto za kufanya kazi nchini Uganda hasa kwa watoto wa kike wenye kupenda kujipodoa na kuvaa nguo zinazoonyesha maumbile basi jua hautaweza kudumu wala kupata kazi nchini humo.Hii ni kutokana na sheria mpya iliyopo, Kwa mujibu wa mtandao wa edaily wa Kenya, umeripoti kuwa serikali ya Uganda imepiga marufuku uvaaji wa nguo fupi makazini, upakaji make up uliozidi, kubandika kucha ndefu na bandia, kuweka nywele bandia na kuzipaka rangi, kuvaa nguo inayobana kama vile Tshirt na magauni pamoja na kuvaa vivalio.

Miaka 2013 nchi hiyo ilitunga sheria ya kukataza kuvaa nguo fupi, sheria ambayo ilizua mijadala nchini humo na sehemu zingine.

Na Laila Sued

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search