Monday, 10 July 2017

TANZIA:MTANGAZAJI WA EFM SETH KITENDE'BIKIRA WA KISUKUMA'AFARIKIRI DUNIA


Seth Kitende enzi za uhai wake

Mtangazaji wa kituo cha radio EFM cha Jijini Dar es salaam ambaye alikuwa anatangaza kipindi cha Ubaoni Seth Katende maarufu kwa jina ‘Bikira wa Kisukuma’ amefariki dunia leo jioni Jumapili Julai 9,2017.

Taarifa za awali zinasema Seth amefariki akiwa kwenye Hospitali ya taifa Muhimbili baada ya kuugua kwa muda mfupi.

Seth Katende alijipatia umaarufu mkubwa kwenye mitandao ya kijamii Tanzania akifahamika kwa jina la ‘Bikira wa Kisukuma’ ambapo baadae alianza kufanya kazi ya Radio kwenye kituo cha EFM.

Msiba upo nyumbani kwa baba yake Changanyikeni Dar es salaam.

motomotonews.com inawapa pole wafanyakazi wa EFM,Waandishi wa Habari Tanzania,ndugu jamaa na marafiki kwa msiba huu. Mungu ailaze mahali pema peponi roho ya marehemu Seth. Amina.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search