Monday, 17 July 2017

UTURUKI: Mwaka mmoja baada ya mapinduzi maafisa 7,000 wa Serikali waachishwa kazi

_96943141_erdogan4.jpg 

Serikali ya Uturuki imewaachisha kazi zaidi ya maafisa 7,000 wa polisi, maafisa wa Serikali na wasomi waliokuwa na uhusiano na jaribio la mapinduzi la mwaka uliopita.

Hatua hii imechukuliwa wakati wa kuadhimisha mwaka wa kwanza tangu jaribiio hilo la mapinduzi kuangamizwa.

Zaidi ya watu 250 waliuawa kabla ya jaribio hilo kuzimwa na wanajeshi walioa waaminifu kwa Serikali.

Hatua hii ni sehemu moja tu ya kuwaondoa watu wasio waaminifu ambapo kufikia sasa zaidi ya watu 200,000 wameachishwa kazi.

Rais Erdogan anawalaumu kwa kuunga mkono wapangaji wa mapinduzi hayo yanayodaiwa kupangwa na kiongozi wa kidini aliye uhamishoni Marekani, Fethullah Gulen.

Bwana Gullen anasema kuwa Rais anasema uongo kuhusiana jaribio na mapinduzi hayo.

Chanzo: BBC

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search