Thursday, 6 July 2017

WATUMISHI WAVIVU SASA KUKATWA MISHAHARA

BUNGE limepitisha Muswada wa Marekebisho ya Sheria Mbalimbali, na sasa sheria imetamka kuwa ofi sa wa umma aliyesababishia serikali au taasisi ya umma kushindwa kutekeleza majukumu yake kwa makusudi au kwa uzembe, atachukuliwa hatua ikiwa ni pamoja na kukatwa mshahara wa miezi sita.

Aidha, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, George Masaju amesema mabadiliko ya Sheria ya Bajeti na yale ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali yaliyopitishwa jana bungeni, hayakusudii kupoka kwa namna yoyote ile mamlaka ya kisheria ya Bunge.

Kifungu cha 65(2) cha Sheria ya Bajeti kinaweka masharti kuwa iwapo itathibitika kuwa ofisa wa umma kwa makusudi au kutokana na uzembe, alisababisha serikali au taasisi ya umma kushindwa kutekeleza majukumu yake chini ya sheria hiyo, atatenda kosa la kinidhamu.

Masaju alisema atawajibishwa binafsi kwa kuchukuliwa hatua za kinidhamu au kushtakiwa kwa kosa la jinai kulingana na aina ya madhara yatokanayo na kushindwa majukumu hayo.

Kuhusu uhamisho wa fedha, alisema baada ya mabadiliko hayo hivi sasa uwasilishaji wa taarifa za uhamisho wa fedha na uwasilishaji wa taarifa za serikali na taarifa za mapato na matumizi, zitawasilishwa kila baada ya miezi sita kwa maana ya nusu mwaka, badala ya miezi mitatu kwa maana ya robo mwaka kama ilivyokuwa awali.

Akihitimisha hoja yake aliyoiwasilisha bungeni kuhusu Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali wa Mwaka 2017, ambayo ndani yake ililenga kufanya mabadiliko katika Sheria ya Bajeti na mabadiliko ya sheria ya ofisi yake, Masaju alisema kimsingi muswada huo sio wa kubadilisha kanuni za haki na madaraka ya Bunge wala madaraka ya Kamati ya Bajeti kama baadhi ya wabunge wanavyodhan

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search