Thursday, 20 July 2017

WIZARA YA MAMBO YA NDANI YAKANUSHA UZUSHI UNAOENDELEA MITANDAONI

nembo 3_thumb[1]
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi inapenda kuujulisha Umma  kuwa kumekuwepo na taarifa za uongo zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii zenye kichwa cha Habari kinachosema “Kanuni/Sheria  za Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Taarifa hizo zimeanza kusambazwa  kuanzia jana tarehe 18 Julai 2017  zikidai kuwa  kuanzia tarehe  19 mwezi Julai  Mwaka 2017 na kuendelea  kutakuwa  kuna Kanuni  mpya za Mawasiliano.
 Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi inapenda kuujulisha Umma  kuwa Taarifa hiyo ni ya uongo na uzushi na haina ukweli wowote na inalenga kuwavuruga wananchi hivyo wananchi waipuuze taarifa hiyo.
Wizara inatoa onyo kali kwa mtu yeyote aliyeanzisha na wale wanaoendelea kusambaza taarifa hiyo na pia hatua kali zitachukuliwa  kwa watu wanaozusha  mambo kwenye mitandao ya kijamii kwa kuwa Serikali inao mfumo rasmi wa utoaji wa taarifa  kwa kutumia mfumo wa “kielectroniki na hardcopy’’.  
Imetolewa na
Christina R. Mwangosi
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali  
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
19 Julai 2017
0712224122/0754817879
christinamwangosi@yahoo.com

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search