Thursday, 20 July 2017

YULE MAMA ALIYEKUTWA MTUPU MCHANA KWEUPE AKIWA NA UNGO AZUA SINTOFAHAMU

TUKIO la mama ambaye jina lake halikupatikana mara moja kukutwa ameketi katikati ya barabara akiwa uchi wa mnyama limezua tafrani na mjadala mkali kufuatia mazingira ya tukio zima huku maswali yakiwa mengi kuliko uhalisia.
Kisanga hicho kilichozua taharuki na zogo kutoka kwa watu, kilijiri jana asubuhi maeneo ya Banana-Ukonga jijini Dar,   hali iliyopelekea kusimama kwa shughuli za kijamii kwa muda.MAZINGIRA YA TUKIO
Mapema asubuhi, wakati watu wakianza ‘mishemishe’ za kuikaribisha siku mpya  mama huyo alionekana ameketi katikati ya barabara, akiwa mtupu na pembeni kukiwa na ungo  na mkoba, jambao lililovuta hisia za wengi na kulazimika kusogea karibu na eneo hilo kushuhudia kwa ukaribu ili kubaini kilichojiri.Ilizidi kudaiwa kuwa mama huyo alisikika akizungumza maneno yasiyoeleweka huku akiwa na kiwewe akijaribu kutafuta namna ya kujisitiri kuondokana na aibu. Kutokana na hali hiyo, baadhi ya akina mama waliingiwa na moyo wa huruma kwa mwanamke mwenzao  na kujitolea mavazi (khanga) na kumsitiri ingawa wengine hususan wanaume walisikika wakizomea na kushangilia huku wakimuita majina yenye tafsiri mbaya.


MJADALA ULIOZUKA
Katika eneo la tukio, yapo maswali makubwa matatu yaliyozua mjadala ambayo yalichangiwa na mazingira husika.

“Mbona mwanamke mwenyewe anaonekana mstaarabu wa kutoendana kabisa na mazingira haya? Lakini pia kama ni mchawi au mwanga mbona anaongea wakati ilivyo kawaida kama mchawi akinaswa akifanya uchawi wake huwa hawaongei hadi ‘wagutuliwe’ tofauti na alivyoonekana mwanzo akizungumza mwenyewe? Lakini pia mbona kuna mkoba, kwani mchawi huwa na mkoba kweli?”   Hayo ni baadhi ya maswali yaliyosikika kutoka kwa watu waliokuwa eneo la tukio, huku yakizua mjadala na sintofahamu yenye fumbo zito.

GPL

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search