Friday, 4 August 2017

AUAWA KWA KUCHOMWA KISA NA MKEWE KUTOKANA NA WIVU WA MAPENZI

MSICHANA mwenye umri wa miaka 25, Janet Mwenda anashikiliwa na Polisi mkoani Mara kwa tuhuma ya kumuua kwa kisu mpenzi wake, Mgini Aaron (37).

Mauaji hayo yalitokea juzi saa 11 jioni katika Kitongoji cha Kitaramanka Kijiji cha Magunga Kata ya Mirwa wilayani Butiama, ambako mtuhumiwa huyo alimchoma kisu hicho katika titi la kushoto na kusababisha kifo cha mpenzi wake huyo.

Akithibitisha mauaji hayo, Kamanda wa Polisi wa Mara, Jafari Mohamed alisema chanzo cha mauaji hayo ni wivu wa mapenzi, baada ya Janet kufika nyumbani akitoka matembezini na kuingia bafuni kuoga na ndipo mpenzi wake alipomtuhumu kwa kumsaliti huko alikotoka.

Kamanda Mohamed alisema Aaron alipoona mpenzi wake akioga, aliona si hali ya kawaida na ndipo alipoanza kumpiga kwa kumtuhumu kusaliti na ndipo mtuhumiwa alipochukua kisu na kumchoma na kusababisha kifo chake. 

Mwili wa marehemu, umehifadhiwa katika hospitali ya mkoa kwa uchunguzi zaidi wa kitabibu.

IMEANDIKWA NA PENDO MWAKYEMBE, BUTIAMA

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search