Monday, 28 August 2017

HATIMAYE JOHARI APATA MPENZI UNAMBIWA MAPENZI YAO MOTOMOTO

Mashallah Johari Atimaye Azama Kwenye Penzi Jipya
Mwigizaji wa kitambo wa tamthiliya na sinema za Kibongo, Blandina Chagula ‘Johari’.

UBUYU wa Zanzibar upo wa aina nyingi. Kuna uliotiwa hiliki, mwingine unachanganywa na mdalasini. Lakini ubuyu wa leo ni ule uliotiwa pilipili mtama na tangawizi. Ukiumung’unya sharti mdomo ukucheze! Upo hapo? Ubuyu huu si mwingine bali ni wa mwigizaji wa kitambo wa tamthiliya na sinema za Kibongo, Blandina Chagula ‘Johari’.
MAHABA SIYO YA NCHI HII
Ubuyu ulionyakwa na safu hii unadai kuwa, Johari kwa sasa amenasa kwenye penzi jipya na jamaa ambaye jina halikupatikana mara moja hivyo linafanyiwa kazi, lakini ishu ni kwamba wanadaiwa kuwa kwenye mahaba mazito ambayo siyo ya nchi hii. Chanzo makini kilichomwaga ubuyu huu kwenye ungo kwa ajili ya watu kujinafasi kilitonya kuwa, Johari na mwanaume huyo anayesemekana ni bonge la mtanashati, huwa mara nyingi wanapenda kujivinjari kwenye ‘pub’ mpya ya mwigizaji matata wa Bongo Movies, Irene Uwoya iitwayo Left Minutes iliyopo maeneo ya Sinza-Mori jijini Dar.

Blandina Chagula ‘Johari’ akiwa na anayedaiwa kuwa mpenzi wake.
JOHARI AMEPATA POZO LA MOYO?
“Unaambiwa bidada Johari sasa hivi amepata pozo la moyo wake. Yaani huyo kaka anampenda Johari hadi raha na hapa nafikiria kabisa wana mpango wa kufunga ndoa. “Ukitaka kujionea mambo mara nyingi utawakuta pale kwenye baa ya Uwoya na muda wote wanapokuwa pamoja wanakuwa kwenye mahabati mazito,” kilinyetisha chanzo hicho kwa sharti la kutotajwa gazetini.

Mnyetishaji huyo alidondosha ubuyu kuwa, mtu ambaye huwa anapenda kuwaweka kwenye ukurasa wake wa Snap Chat ni Uwoya ambaye anaonekana kuubariki uhusiano huo. Ijumaa Wikienda, kama kawaida yake, baada ya kupata ubuyu huo mtamu lilifunga safari hadi kwenye baa ya Uwoya na kuzungumza na ‘mashushushu’ wake ambao walikiri kumuona staa huyo na ‘bebi’ wake huyo mpya (new brand).


Baada ya Ijumaa Wikienda lilimtafuta Uwoya ambaye anatajwa kuwa ‘kiunganishi’ na msiri mkubwa wa Johari na pia anawaposti kwenye mtandao ili aweze kufafanua juu ya kinachoendelea. Katika majibu yake, Uwoya hakukataa wala kukiri kuwepo kwa uhusiano huo, lakini alisema yeye hawezi kujua hata siku moja kitu ambacho kipo mioyoni mwa watu. “Jamani kwani mimi siruhusiwi kumposti mtu picha yake akiwa hata na jamaa yake? Maana hao kama wana uhusiano wa kimapenzi mimi sina uhakika na hilo,” alisema Uwoya.

Ijumaa Wikienda halikuishia hapo, bali lilifunga safari kumsaka Johari ili kumfungukia mwanaume huyo ambapo mambo yalikuwa hivi; Ijumaa
Wikienda: Mambo Johari, vipi kuhusu mipango ya ndoa na shemeji yetu mpya?

Johari: Shemeji? Yupi huyo tena?
Ijumaa Wikienda: Kwani wapo wangapi wapya? Namaanisha huyo unayejiachia naye kwenye baa ya Uwoya na kujiachia.

Johari: Jamani…mhhh…hapana… huyo siyo mtu wangu mimi. Ijumaa Wikienda: Mbona mnaonekana mkiwa kwenye mahaba mazito?

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search