Tuesday, 15 August 2017

HAYA NI MATATIZO YA MIMBA AMBAYO HUTOKEA KATI YA WIKI 1 MPAKA 12

Matatizo ya mimba wiki 1 hadi 12
1. Mimba kutoka, hali hii mara nyingi hutokea wiki za mwanzo za mimba... sababu zipo mbalimbali ila moja kubwa... mimba inaweza kutungwa bila kukamilika hivyo mwili unaikataa.
2. Mama anakuwa na damu ambayo inapingana na damu ya mtoto ( mfano Mama ni group A- na mtoto ni grouo AB + ) mfano Baba ni B+ na Mama ni A-... ( soma post zilizopita utaelewa hili vizuri zaidi)
hii hapa ikigundulika hutibiwa kwa Mama kuchoma Sindano maalumu kila akijifungua
3. mimba kutungwa vizuri lakini shingo ya kizazi inakuwa haina nguvu, hii hupelekea mimba kutoka. mara nyingi mimba hizi hutoka kuanzia wiki ya 16 na kuendelea. Mama akigundulika anaweza akatibiwa na mimba ikakua hadi akajifungua
4. kuna wakat mama anaweza akawa na mimba, na ikawa kitoto kimefariki... kuna sababu nyingi za mtoto kufariki mapema hivi na mimba kutoka... baadhi ni kama homones kutokubalansi, vijinasaba ( chromosomes ) kukosea katika kutunga mtoto, hali ya mji wa uzazi ( magonjwa mfano endometriosis ) au mfumo wa damu kuganda kuwa na tatizo,
mtoto akifariki hii mimba hutoka na isipotoka wakat wa ultrasound itagundulika na mama atazalishwa.
5. Mimba kutungwa nje ya uzazi. hii mara nyingi haikui hadi mtoto kuzaliwa. huwa kadiri siku zinavyoongeza mama anapata maumivu makali sana eneo la upande mmoja wa kinena. akienda hospital akifanyiwa uchunguzi hugubdulika na hutibiwa kwa kuitoa mimba.
NB mara nyingi hizi mimba nje ya kizazi, mama hugundua wakat ambao mirija ya falolian imechanika na hapo damu inatoka ndani kwa ndani. akifika hospital hutibiwa kwa op na kupona.
6. SIKIA.. mama ambaye anazembea hapa akakimbilia kwa mganga wa kienyeji au kwenye maombi kadiri atakavyochelewa ni kadiri uhatari unaongezeka. na hata kifo.
hapa nataka kusema kuwa mtu akiumwa aanzie kwenda hospital alafu maombi yafate.
7. dalili hizi zikitokea wakat wa mwanzo wa mimba wahi hospital.
kutokwa na damu...
kuwa na homa kali
maumivu makali eneo la kinena
maumivu makal wakat wa kukojoa
kuvimba mguu au miguu yote,
kichwa kuuma sana
kizunguzungu
kutapika sana ( zaidi ya mara 5 kwa siku )
post ijayo itaelezea kwa kinagaubaga umuhimu wa mazoezi wakat wa mimba.. na lini mtu aanze mazoezi...
Share ili mwenzako afaidi pia.
Imeandikwa na Dk Paulo Matemu

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search