Tuesday, 29 August 2017

HII NI TAARIFA YA AWALI YA UCHUNGUZI YA POLISI KUHUSU KILICHOSABABISHA MLIPUKO KWENYE OFISI YA IMMMA ADVOCATES

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, leo limesema kuwa uchunguzi wa awali umebaini kuwa watu wasiojulikana utambulisho wao na idadi yao walifika katika ofisi za Mawakili wa IMMMA Advocates wakiwa katika magari mawili na kujifanya ni maaskari na kuwarubuni walinzi na kuondoka nao katika gari mojawapo kabla ya kulipua jengo hilo.


Walinzi hao wanadaiwa kukutwa baadaye maeneo ya Kawe wakiwa hawajitambui.


Imedaiwa kuwa kundi lililobaki liliingia katika ofisi hizo hilo na kuweka vilipuzi vilivyotengenezwa kienyeji, ambavyo vililipuka muda mfupi baada ya watu hao kuondoka eneo hilo na kusababisha uharibifu wa wa mali na jengo la ofisi hiyo pamoja na majengo ya jirani.


Jeshi hilo limesema kuwa linaendelea kufanya uchunguzi wa kina ili kubaini watu waliofanya tukio hilo na kujua dhamira yao ili wafikishwe katika vyombo vya sheria kwani wajibu wa jeshi la polisi ni kulinda raia na mali zao na kamwe haliwezi kuhujumu maisha ya watu na mali za wananchiAidha, jeshi hilo limewaomba waathirika wa tukio hilo na wananchi kwa ujumla kuwa watulivu wakati vyombo vya dola vikiendelea na upelelezi wa tukio hilo

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search