Thursday, 17 August 2017

INASIKITISHA SANA-MWANAUME AMUUA MPENZI WAKE KISHA NA YEYE KUJIUA DAR ES SALAAM


Binti mmoja aliyefahamika kwa jina la Maria Pius amezikwa leo makaburi ya Mwananyamala kwa Kopa baada ya mpenzi wake kumuua kwa kumpiga na kitu chenye nchi kali kisha mwili wake kuutupa kwenye shamba huko Chanika jijini Dar es Salaam.


Inasemekana siku ya Jumatatu mwanaume huyo ambaye jina lake halijafahamika alimpiga binti huyo na vitu vyenye ncha kali kwa kinachoelezwa kuwa ni wivu wa mapenzi mpaka alipopoteza maisha kisha muaji huyo aliandika ujumbe unaosema wasimatafute muuaji kwani amemuua yeye, kisha ujumbe huo aliuweka kwenye kifua cha binti huyo pamoja na simu mbili, simu ya mtuhumiwa pamoja na simu ya binti huyo.


Baada ya watu kugundua kuwa binti huyo ameuawa na kutoa taarifa kwenye vyombo vya dola inadaiwa siku ya kesho yake ambayo ni jana mwanaume huyo aliyedaiwa kufanya mauaji hayo naye aliamua kujitoa uhai kwa kujitumbukiza kwenye kisima cha maji na kupoteza maisha.Baadhi ya ndugu na majirani wa binti huyo waliopo Mwananyamala sehemu ambayo alikuwa akiishi kabla ya kwenda huko Chanika na kuanza maisha na mwanaume huyo wamesema binti huyo alikuwa anaishi na mwanaume huyo Chanika lakini mwanaume huyo walikuwa hawamfahamu kwani hajawahi kujitambulisha kwao na wala binti huyo hajawahi kumpeleka.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search