Friday, 18 August 2017

KANUNI HIZI 7 NI MUHIMU SANA KATIKA MAMBO YA UPATANISHO WA MAHUSIANO UKIZIFUATA UTAISHI KWA AMANI NA MWENZI WAKO

Na Abilius Wamara.
Tofauti katika mahusiano ni jambo ambalo halikwepeki na hakuna mahusiano yasiyo kuwa na tofauti.

Pindi watu waliokatika mahusiano wanapotofautiana ni bora wakazijua kanuni hizi.

1. Watambue neno SAMAHANI halina jinsia
Aliyekosea ndiye aombe kusamehewa hili halijalushi ni mme au mke. Ubabe katika mahusiano si njia bora ya kumaliza tofauti zenu.

2. Tabia ya kususa susa siyo nzuri
Wengine wakisha tofautiana hususa wakidhani ndo wanatatua tofauti zao....wengine hususa kuongea, wengine hususa kula na mbaya zaidi wengine hususia hadi huduma ya kitandani ambao ndio nguzo muhimu katika mahusiano.

3. Ugomvi unaoanzia chumbani umalizikie kitandani
Ugomvi mliouanzia chumbani uishie chumbani hukohuko na usitoke nje. ........walio katika mahusiano wajitahidi kusikilizana na kutatua tofauti zao wenyewe na zaidi kitanda kiwe jukwaa la upatanishi na siyo vinginevyo.

4. Mmoja lazima akubali kuumia ili mwenzie apate amani
Jifunze kushuka( sometimes calm down) hii itakusaidia kurejesha amani katika mahusiano yako. Usipandishe sauti wakati unamwona mwenzio naye yuko juu na kajawa na hasira. Kwa kujishusha amani irarejea tu.

5. Acha mawazo ya kuachika
Huyo ni wako zaidi waza urejesho na siyo uharibifu. Mlikubaliana mkapatana na mkayaanzisha mahusiano. Usivunje mahusiano uliyoyajenga kwa muda na ghsrama kubwa kwa jambo dogo sana. Talaka haijawahi kumwacha mtu salama.

6. Samehe, Achilia na Mchukulie mwenzio
Hakuna aliye mkamilifu katika dunia hii.  Sisi wote tuna madhaifu (weekness) unapoona mahusiano yamedumu ujue hao wamefuzu kiwango cha juu cha kuvumiliana na kuchukuliana.

7. Jenga utaratibu wa kufanya ibada pamoja
Sote tunajua mpatanishi mkuu ni mwenyezi Mungu. Hivyo mnapounganisha mikono yenu kwa pamoja na mkamuita Mungu awasaidie hakika mnakuwa sehemu salama kuliko ukifanya vinginevyo. Mahusiano yanayomtegemea Mungu kamwe huwa hayateteleki.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search