Friday, 4 August 2017

KWA WADADA SOMENI HUU UJUMBE MUHIMU SANA

"WAAMBIE NA WENZAKO………
Wewe ni msichana mzuri, unapenda kwenda na wakati. Umeshaanza kutumia vilevi. Tena vile laini ambavyo ukinywa leo unaweza kulewa kesho.
Una mahusiano na John. Lakini unampenda sana Simon. Japo mvulana aliyekutoa bikira ni Side lakini toka muachane humuhitaji tena kwakua unamuona mshamba na unaona kabisa kua ulikosea njia kuwa nae.
Sponsor Molito ni baba unaye muheshimu sana. Kwakua uki date nae tu basi unarudi na mkwanja mrefu nyumbani.
John hana pesa nyingi, ila bishoo. Ana Dred na kifua kipana. Anashinda gym kwa sababu yako ili u enjoy ukiwa nae.
Simon ndio mvulana anaye julikana na rafiki zako wengi kwakua ndio mvulana ambaye unashinda nae muda mrefu. Hivyo umemuaminisha kua unampenda yeye peke yake.
Simon ndio mvulana ambaye unaweza hata kumpost kwenye mitandao lakini Caption zako za kawaida sana zisizoonyesha dalili zozote za mahusiano.
Upo na marafiki zako wapatao wanne ambao wote life style yenu ndio hiyo.
Kila mkilala mchana mnawaza usiku muende club gani au wapi kuna pub nzuri ili mlewe.
Unaishi na mama yako na wadogo zako wanasoma. Mama hana usemi kwako kwakua ukitoka kwa Sponsor Molito unamtupia laki 2.
Mama anakuruhusu ukapumzike. Na simu yako ikiita anakuletea ndani na kukuamsha kwa adabu. Kiufupi mama yako hana kauli juu yako kwakua wewe ndio tegemezi.
Shopping yako ni laki 3 kwenda mbele. Hurudii nguo mara tatu. Usisikie simu mpya imetoka. Tayari unayo. Kwenu hamna gari lakini umeshajifunza na unatembelea magari Zaidi ya matatu lakini huna kadi hata moja.
Umepanga nyumba nzima na huna kazi mjini. Ofisi yako ni simu na sauti nzuri ya kutokea puani.
Miaka haisubiri. Ulikua na miaka 20 na miaka saba baadae unakua na miaka 27.
Hushtuki. Poda zinaanza kudunda na vipodozi vinaanza kukataa kushika kwenye ngozi yako.
Unaamua kubadilisha cream na kutumia zile kali kali ili ngozi ikubali.
Unakua mweupe sana. Macho nayo yanapoteza nuru. Huwezi tembea kwenye jua kali. Muda wote kope za bandia ndio mlinzi wa muonekano wako.
Sponsor Molito nae anahitaji kuwa na watoto wabichi wa miaka 20. Wewe age imeshakutupa mkono. Anakuona wa kawaida. Huna maajabu tena.


Anakuacha na kukupa wakati mgumu wa kutafuta Sponsor mwengine.
Inakua ngumu kuwapata kwa natural face, unaanza kufanya photoshoot za nusu uchi na editing nyingi ili wachuuzi wanase.
Wananasa watoto wa facebook na Instagram wafuga dread na wanyoa viduku. Hao huwataki.
Stress zinapanda unaanza kumlazimisha Simon akave nafasi ya Molito. Simon hana uwezo. Unampiga chini unabaki na Serengeti boy wako John.
Huyo anapendwa na wasichana wengi, unamfumania na kuachana nae kwa matusi.
Unabaki Single, huna danga wala bwana. Rafiki zako ukiwapigia simu ni vizinga tu na kuwaomba wakutoe out.. huna Ishu. Unalala tu usiku wakati ulikua unajiita POPO.
Rafiki zako wanakupitia na magari yao ambayo hawana kadi nayo wanakutoa. mkitoka ni wao tu ndio wanatumia pesa zao. Baada ya muda wanakuchoka, Wanaanza kukutenga na kukuzimia simu.
Huwezi panda daladala kwakua mtaani unaitwa Cash Madame. Unaanza kupanda pikipiki kila mahali uendapo. Huna pesa za kulipia usafiri kila siku.
Unaamua kutembea na dereva boda boda ili upate usafiri wa bure.
Huyo hakutoshi kwakua wewe una gaharama sana.
Unaamua kumpa penzi mangi wa dukani ili vitu vidogodogo uwe unachukua bure,
Mangi hana siri, anakutangazia kuwa unamtaka na kuwa skendo kwako.
Unaamua kujifungia ndani skendo ipite.
Laahaulaaaaaaaaa!
Unakuja Kutahamaki. Unafungua friji kuna maji tu, dawa ya meno imeisha, Gesi imaisha, luku nayo inakaribia kuisha, dukani kwa shirima mnadaiwa laki 2. Kodi ya nyumba inakaribia. Unamuita baba mwenye nyumba unampa penzi. Anakuongeza miezi mitatu……
Kuja kutahamaki wewe unaishi kwa kufanya mapenzi na kila aina ya mtu kwakua tu umeamua ku fake maisha yako.
Yanini yote dada zangu?
Jikubali kua wewe unaweza kutoka kimaisha na kuisaidia familia yako kwa njia salama kabisa bila kuutumia mwili wako.
Hayo madanga huwa hayazeeki bali wewe unayedanga ndio unapitwa na wakati.
Hayo madanga wanapenda wasichina wenye miaka ishirini.
Wewe ukipita basi atatafuntwa mwengine. Utaishia kutunza makabati ya kichina wenzako wakiolewa na wewe ukabaki na uzuri wako wa dukani.
Badilikine.. Ikimkera mtu naandaa nyingine……"
@ *PAMBANA* *NA HALI YAKO*

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search