Friday, 4 August 2017

MAHAKAMA YAAMURU WABUNGE 8 WAPYA WA CUF WAAPISHWE

Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam leo August 4, 2017 imetupilia mbali pingamizi la Wabunge 8 wa Viti Maalumu waliofutwa uanachama na Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF Prof. Ibrahim Lipumba ya kutaka wabunge wateule 8 wasiapishwe na Bunge.Uamuzi huo, umetolewa na Jaji Lugano Mwandambo ambaye amesema ametupilia mbali pingamizi hilo la zuio la kuapishwa kwa Wabunge hao 8 na kwa mantiki hiyo, Wabunge wapya walioteuliwa kuziba nafasi zao wanaweza kuapishwa.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search