Tuesday, 29 August 2017

Rais Magufuli aitaka TAKUKURU kuwachukulia hatua wote wanaojihusisha na rushwa pale wanapokuwa na ushahidi

Rais John Magufuli amewataka viongozi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kutokuwa na kigugumizi cha kuchukua hatua pale wanapokuwa na ushahidi dhidi ya watu wanaojihusisha na vitendo vya rushwa.

Ametoa agizo hilo leo Agosti 28, alipotembelea na kuzungumza na wafanyakazi wa Takukuru katika ofisi za makao makuu ya Taasisi hiyo jijini Dar es Salaam.

“Kuna mambo mengi ya hovyo yanafanyika, tumehakiki pembejeo za ruzuku na kubaini madai ya Sh48 bilioni ni hewa, tumebaini wafanyakazi hewa zaidi ya 19,500, tumebaini kaya masikini hewa 56,000 zilizopaswa kupata fedha Tasaf, tumebaini wanafunzi hewa 5,850 waliotakiwa kupata mkopo, kuna vichwa vya treni 11 vimeletwa bila kuwepo mkataba na mengine mengi, haya yote yanafanyika kwa rushwa, nataka kuwaona mnachukua hatua stahiki,”amesema.

Taarifa ya Ikulu imesema Rais ameeleza kuwa na imani na Takukuru na amewataka wafanyakazi wake kufanya kazi kwa kuzingatia weledi, uzalendo na uadilifu, akiahidi Serikali kufanyia kazi changamoto zinazowakabili.

ikulu1.jpg ikulu2.jpg

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search