Wednesday, 9 August 2017

REAL MADRID WASHINDA UBINGWA WA UEFA SUPER CUP YAIRARUA MAN UTD 2-1 NA KUBEBA KOMBE

 Usiku wa August 8 2017 mchezo ambao ulikuwa ukisubiriwa kwa hamu wa UEFA Super Cup kati ya Bingwa wa UEFA Champions League Real Madrid dhidi ya Bingwa wa Europa League Man United ulichezwa katika uwanja wa Nacionalna Arena.

Real Madrid ambao walianza game bila uwepo wa staa wao Cristiano Ronaldo aliyeingia dakika 8 za mwisho, wamefanikiwa kupata Ubingwa wa UEFA Super Cup kwa kuifunga Man United kwa magoli 2-1, magoli ya Real yakifungwa na Casemiro dakika 24, Isco dakika ya 52 na Man United walipata goli la kufutia machozi kupitia kwa Romelu Lukaku dakika ya 62.


Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search