Thursday, 17 August 2017

WANAFUNZI WA SHULE YA MIRAMBO TABORA WAPATAO 106 WAKAMATWA KWA KUFANYA VURUGU KWENYE HARUSI

Jeshi la Polisi mkoani Tabora linawashikilia wanafunzi 106 wa shule ya Sekondari ya Milambo kwa madai ya kufanya vurugu na kujeruhi wananchi zaidi ya sita katika eneo la jirani na shule hiyo.Wanafunzi hao wa kidato cha sita wamefanya vurugu hizo usiku baada ya kutoroka shuleni na kuvamia kwenye sherehe ya harusi ambapo walitaka sherehe hiyo iendelee hadi muda watakao amua wao.

Akizungumzia tukio hilo, Kamanda wa Polisi mkoani humo, SACP Wilbroad Mutafungwa amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo ameeleza kuwa wanafunzi hao 106 wanashikiliwa na jeshi la polisi kuhusiana na tukio hilo.
Tazama tukio hilo hapo chini

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search