Thursday, 7 September 2017

BREAKING NEWS:NAIBU WAZIRI EDWIN NGANYANI AJIUZULU KUFUATIA SAKATA LA MAKINIKIA YA ALMASI

Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Edwin Ngonyani amesema anaandika barua ya kujiuzulu baada ya Rais John Magufuli kuwataka watu wote waliotajwa kwenye ripoti ya biashara ya madini ya almasi na Tanzanite kujiondoa wenyewe.
Akiongea leo Alhamis mchana mara baada ya hafla ya makabidhianao ya ripoti hizo, Ngonyani amesema amepokea kauli ya Rais kwa mikono miwili na sasa anaandika barua ya kujiuzulu nafasi hiyo.
“Hata sasa unanichelewesha nipo naandika barua ya kujiuzulu, hii ni nafasi niliyopewa na ni lazima nimuunge mkono Rais katika hatua zake za kutaka kubadili mfumo wa nchi na kuufanya wenye manufaa kwa wananchi,” amesema Ngonyani.
Amesema hawezi kuongeza chochote juu ya kauli ya Rais na anaviachia kazi vyombo vya ulinzi na usalama kufanya kazi yake kama ambavyo mkuu wa nchi amevitaka.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search