Tuesday, 19 September 2017

DIAMOND AKUBALI MTOTO WA HAMISA KUWA NI WAKE


Diamond Aliamsha Dude Afunguka Kuzaa na Hamisa Mobetto Asema Nilitaka Mwanangu Aitwe Dylan

Mwanamuziki Diamond Platnumz amesema jina alilotoa apewe mtoto wake kwa Hamisa Mobetto ni Dylan lakini kwa sababu za kutafuta umaarufu mwanamke huyo alimwita Abdul Nassib.

Amesema Hamisa alimwita mtoto huyo Abdul ambalo ni jina la baba yake mzazi ili iwe rahisi watu kufahamu kuwa mtoto huyo ni wa kwake baada ya kukubaliana kufanya uhusiano wao kuwa wa siri.

“Mimi jina ninalolitambua ni Dylan hata niliposikia wamemwita Abdul nilisema poa tu lakini akija kwangu nitamwita ninalolitaka mimi kwa sababu nataka aitwe DD (D Square).”

Amesema alisikitishwa pia na kitendo cha mwanamke huyo kumualika baba yake katika sherehe ya kutimiza siku arobaini ya mtoto huyo akimdanganya kuwa angekuwepo.

“Walimwalika mzee Abdul na nguo wakampelekea ili ahudhurie, yote hiyo ili mradi tu wapate cha kuzungumziwa mitandaoni,” amesema.


“Mimba ni yangu na sitokaa nikaachana na Zari,” amesema Platnumz.

Ambapo amesema amemgharamia Hamisa pamoja na mtoto tangu kipindi cha ujauzito wake mpaka mtoto anazaliwa ili kuhakikisha mama na mtoto huyo wanakuwa salama.

Amesema pamoja na yaliyotokea alimwambia mama yake mzazi kuhusu kilichotokea amemuomba msamaha Zari na hawana shida yoyote.

“Mimi ni mwanadamu na kilichotokea kimetokea na niko tayari kumhudumia mtoto,” amesema Diamond.

Diamond amesema kuwa alimuonya Hamisa kutokumtukana Zari kwani hausiki na chochote kilichotokea na badala yake ajishughulishe na mambo mengine

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search