Tuesday, 5 September 2017

FURGESON :NILIWAPA UHURU WACHEZAJI WAKUBWA KUMCHEZEA FAULO CRISTIANO RONALDO

Mwanasoka bora wa dunia Cristiano Ronaldo aliwahi kusema kwamba Sir Alex Ferguson ni baba yake, hii ilitokana na mahusiano ya karibu yaliyopo baina ya mchezaji huyo na kocha Ferguson.
Ferguson ndiye alimnunua Cristiano toka Sporting ya nchini Ureno na kumuonesha anamuamini aliamua kumpa jezi namba 7 ambayo ni jezi inayovaliwa na wachezaji wakubwa wakifika United.
Toka ajiunge na United Ronaldo amekuwa akikua kisoka siku hadi siku lakini kumbe nyuma ya pazia kuna siri ilifichika juu ya uara wa Cristiano Ronaldo na ushupavu wake anapokuwa uwanjani.
Kocha msaidizi wa zamani wa Manchester United Tonny Coton amesema Ferguson aliwaambia makocha wasaidizi kukaa kimya pale Ronaldo anapofanyiwa faulu na kuacha mpira uendelee.
“Wakati anakuja alikuwa anapenda kujiangusha na kulala lala wakati akichezewa faulu, Ferguson aliliona hilo ndipo alituambia tuwe kama hatuoni akichezewa faulu ili kumfanya akomae na aache kulala lala” alisema Coton.
Coton anasema idea hii ya Ferguson iliwafanya baadhi ya walinzi wakorofi kama Roy Keane na Rio Ferdinand kumchezea rafu Ronaldo, lakini pamoja na rafu hizo hakuna kocha aliyejali bali mpira uliendelea kama kawaida na Cr7 akibaki ananyoosha tu mikono.
Toka Fergie amfanyie hivyo Cristiano kilichofuatia ilikuwa hadithi tamu tu kwa Ronaldo kwani tangu wakati huo hadi sasa mchezaji huyo ameshashinda karibu kila kitu katika ngazi ya klabu.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search