Tuesday, 5 September 2017

HAYA HAPA MATOKEO YA MECHI ZA KUFUZU KOMBE LA DUNIA -MECHI ZILIZOCHEZWA JANA JUMATATU

Dakika ya 3 tu ya mchezo kati ya England na Slovakia mshambuliaji wa Manchester United Marcus Rashford alitoa boko ambalo liliigharimu Uingereza na Slovakia wakapata bao la kuongoza kupitia kwa Stainsliv Lobokta.
Lakini Rashford dakika ya 37 alirekebisha makosa kwa kutoa assist ya bao la Eric Dier na kama hiyo haitoshi Marcus Rashford dakika ya 59 aliipatia bao la pili na la ushindi kwa timu ya taifa ya Uingereza, na kuifanya Uingereza kutopoteza michezo 37 ya kufudhu kombe la dunia.
Wajerumani waliifunga Norway bao 6 kwa nunge huku Timl Werner akifunga mara mbili, Mario Gomez, Julian Draxler, Mario Gomez na Leon Goreztka kufunga bao moja moja.
Robert Lewandoski alifunga moja ya bao wakati Poland wakiizamisha timu ya taifa ya Kazakhstan mabao 3 kwa nunge huku mengine yakifungwa na Kamil Glik na Arkadiusz Milik.
Nigeria wakiwa ugenini waliilazimisha Cameroon sare ya bao moja kwa moja huku bao la Nigeria likifungwa na Moses Simon na Cameroon wakisawazisha kwa mkwaju wa penati dakika ya 75 kupitia Vicent Aboubakar.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search