Monday, 4 September 2017

Haya ni Mambo 7 Muhimu Yanayoonyesha Wewe na Mpenzi Wako Mna Uhusiano Imara

Mambo 7 Yanayoonyesha Wewe na Mpenzi Wako Mna Uhusiano Imara

Haijalishi ni kwa namna gani uhusiano umeanza au umeisha, kila mara tunapokuwa katika uhusiano lazima kuna somo tunajifunza.

Hakuna uhusiano ambao ni mkamilifu, lazima mtazozana kwa maneno au vitendo na wakati mwingine kugombana kabisa. Lakini kuzonazna huko hakumaanishi kwa uhusiano wenu umefikia mwisho, japokuwa mkiwa watu wa kugombana kila siku, inabidi mkae chini mzungumze kuweza kufahamu tatizo ni nini.

Kuwa na furaha ni jambo moja, lakini kujua kuwa upo katika uhusiano ambao utadumu licha ya kuwa mnapitia magumu kiasi gani, ni jambo jingine ambalo kila mmoja analitamani.

Hapa chini ni ishara saba ambazo zinazungumza kuhusu uimara wa uhusiano wenu.

Mawasiliano
Kikubwa ni kujiuliza mnazungumza kuhusu nini na mna mazungumzo ya aina gani. Manaweza mkawa mnazungumza kuhusu jinsi ya kufanya maamuzi, tabia nzuri amba mbaya zinazowakera au kuhusu maisha yenu ya mbeleni.

Chagua muda sahihi na mahala sahihi pakuzungumzia jambo lako, dunia haitaisha kama ukiamua kusubiri saa moja ili uweze kupata sehemu sahihi ya kuzungumza na mwenza wako. Fahamu unataka kusema nini, utakavyokisema na mazingira utakayosemea ili kuwa na mawasiliano madhubuti.

Makubaliano
Hii sio kwenye uhusiano wa kimapenzi pekee, hata kwa rafiki wa kawaida ni muhimu kuzingatia hili kwani huwezi ukawa kila mara wewe unapokea tu, lazima pawepo wakati wa wewe kutoa pia.

Mnapoingia katika uhusiano, kila mmoja huwa na tabia zake na uelewa wake juu ya mambo, lakini wapenzi ambao ni imara, watakaa na kujadili kuona namna bora ya kuweza kuchanganya tabia zao na kutoka na moja ambayo wote wataikubvali.

Ukiwa wewe hutaki kubadilika ila unataka mwenzako ndio kila mara abadilike kufuata mawazo yako, hakika kila mara mtaishia kugombana.

Uaminifu na kusamehe
Vitu hivi viwili ni muhimu sana katika uhusiano wako, kila mmoja anatakiwa kuweka nguvu sawa kuhakikisha vinaendelea kuwa nguzo muhimu kati yenu wawili. Usiwe na nafasi ya kuwa na mawazo hasi na mwenzako, na unapokuwa na wasiwasi, mwambie na yeye akueleza ukweli pasi na kupepesa macho.

Jifunze kusamehe na kusahau, haiwezekani kwenye uhusiano kila mara nyie mkawa ni watu wa kugombana tu, mtapata wapi muda wa kufurahia uwepo wa mwenzio? Samehe na sahau vitu ambavyo hamuwezi mkaendelea kuvijadili. Haiwezekani mkawa mnaendelea kujadili tatizo lililotokea mwezi uliopita.

Jitambue
Hili huwakumba zaidi wanawake. Wanapoanza kuwa kwenye uhusiano, wapenzi wao huwa ndio dunia yao.  Huwapoteza marafiki zao na kuacha kufanya vile vitu alivyokuwa akivipenda, na badala yake sasa anafanya vitu ambavyo mpenzi wake anavipenda.

Hii huwa haitokei sana kwa wanaume, ni mara chache sana utakuta mwanaume ameacha kuangali mpira kwa sababu tu mpenzi wake hapendi aangalie.

Hakikisha unaendelea kuwa na marafiki, na kufanya vitu ulivyokuwa ukivipenda hata baada ya kuwa kwenye uhusiano. Hivyo vitakusaidia wewe endapo chochote kitatokea katika uhusiano wenu. Hata ikitokea mkaachana na huyo mpenzi wako, bado una marafiki wa kukusaidia.

Wanahitaji kuwa kwenye Maisha yako
Hakuna mtu anayekuwaga ‘busy’ akashindwa kufanya kile anachokipenda. Kama kweli mpenzi wako anakupenda, atatafuta muda kwa ajili yako bila kujali ametingwa kiasi gani kwa sababu tu anakupenda.

Na anapotenga muda kwa ajili yako, mkiwa pamoja awepo pale kiakili na kimwili, sio mwingine akifika anaanza kuchezea simu yake na hakuna kuongeleshana.

Anakufanya ujisikie vizuri na mwenye furaha
Sio lazima uwe umejiremba ndio mpenzi wako aonyeshe kuvutiwa na wewe, hata kama ndio umeamka kutoka usingizi au umetoka kuoga na hujajiremba avutiwe na jinsi ulivyo na hicho kitakufanya ujiamnini na kujiona upo kwenye mikono salama.

Kuwa na mtu ambaye anakuthamini, anayeijua thamani yako, anayeyaweka mawazo yako mbele na  akikosea hasiti kuomba msamaha, mtu ambaye ukiwa naye unajisikia Amani kuliko ukiwa na mwingine yeyote.

 Kuwa wachangamfu (having fun)
Uhusiano wako ni salama, mpenzi wako ni msaidizi wako, uhusiano wako ni mbingu ndogo hapa duniani hauna haja ya kujificha na kutojionyesha wewe ni nani (the real you) ili tu mwenza kwako akukubali.

Ni ninyi wawili tu duniani, Hakuna mwingine, hivyo mnapokuwa na nafasi, furahini, kila mmoja awe huru kwa mwenzake.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search