Saturday, 9 September 2017

HII NDIO TAREHE SHILOLE ATAFUNGA NDOA

Shilole Ametangaza Ndoa Yake  na Uchebe Desemba 20 Mwaka Huu
Hatimaye nyota wa filamu na muziki nchini, Zuwena Mohammed maarufu kama Shilole ametangaza kuwa atafunga ndoa mwishoni mwa mwaka huu.

Shilole amesema atafunga ndoa na mpenzi wake wa sasa Ashraf Uchebe  Desema 20 siku ambayo  ataadhimisha siku yake ya kuzaliwa.

Kauli hiyo imekuja siku chache baada ya kuibuka utata kufuatia akaunti moja ya Instagram inayosomeka jina la Uchebe kuandika maneno ya kumkejeli mwanamuziki huyo.

Shilole ameeleza kuwa akaunti hiyo si ya mpenzi wake bali imetengenezwa na watu wasiowatakia mema.

 "Mpenzi wangu hana akaunti,  watu wanataka kutuharibia sasa nawaambia wameshindwa na tunafunga ndoa," amesema Shilole.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search