Friday, 8 September 2017

HII NDIYO TAARIFA KUHUSU MAENDELEO YA AFYA YA MH TUNDU LISSU


Mwenyekiti wa CHADEMA Mh Freeman Mbowe amefunguka na kuelezea hali ya Mbunge wa Singida Mashariki na kusema mbunge huyo ameumizwa vibaya na kuwa hali yake toka saa nne za asubuhi leo haikuwa vizuri kutokana na majeraha aliyopata.

Mbowe amesema kuwa Mbunge huyo mpaka sasa bado yupo kwenye chumba cha upasuaji katika hospitali ya Nairobi nchini Kenya akiendelea kupatiwa matibabu kufuatia kiongozi huyo kupigwa risasi jana na watu wasiofahamika akiwa mjini Dodoma.

Aidha Mbunge wa Iringa Mjini Peter Msigwa ambaye naye yupo nchini Kenya amelezea hali ilivyokuwa toka walipofika jana usiku nchini Kenya mpaka dakika za mwisho Mbunge huyo alipoingia kwenye chumba cha upasuaji.

"Mh Tundu Lisu aliwasili usiku majira ya saa saba hapa Nairobi Jomo Kenyatta International Airport na alipokelewa na team ya Madaktari wa Nairobi hospital pale Aairport na matibabu yalianza mara moja kuanzia ndani ya Ambulance hadi hospital. Aidha alipofika Nairobi hospital alifanyiwa vipimo vyote na baadae saa nne asubuhi aliingizwa chumba cha upasuaji" aliandika Peter Msigwa kwenye ukurasa wake wa facebook.

Mchungaji Msingwa aliendelea kusema kuwa " Tangu jana alipofika alifanyiwa stabilization ili aweze kukabiliana na surgery na zoezi hilo lilifanikiwa vizuri na madaktari wametueleza kuwa hakuna hali yoyote ya hatari na matibabu yake yanaendelea kwa mafanikio hadi sasa majira ya saa 9 alasiri bado hajatoka theatre na madaktari wametueleza kuwa wanaendelea vizuri"

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search