Monday, 4 September 2017

HIZI NI AINA KUMI ZA NDOA JE WEWE MWANANDOA UKO NAMBA ANGAPI

1.NDOA YA MKEKA.
```Inatokana na kufumaniwa na Binti wa watu. Ndoa hii huwa Haina mahari. Hii huvunjika mwaka mmoja tu baada ya wanandoa kugundua hawakuwa wakipendana!```
2.NDOA YA MIHEMKO (NYEGE).
```Hufungwa na vijana wenye umri wa miaka kati mume18-20 mke 16-19. Huvunjika baada ya miaka 3 au 4 ya ndoa. Hawa huachana na viapo na ikitokea wakaoa au kuolewa basi kidume kitaoa jimama lililomzidi umri na binti atakuwa wa ving'asti maisha```
4.NDOA YA MAONYESHO.
```Wenye ndoa Hii hupenda kujionyesha barabarani, Mitaani, Makanisani, Harusini, Misibani nk. nk. Ila ndani hazina utii. Hupigana kila wanaporudi kutoka kwenye mizunguko yao! Kwa kuchepuka hao ngoma drop!
Cha kushangaza huwa hazivunjiki lakini ndiyo ndoa zinazoongoza kwa Watoto wa vibarazani!```
5.NDOA YA UHAMISHO.
```Hufungwa na watumishi wa Vijijini na Mijini. Ili wa kijijini ahamie mjini. Mahari hutoa anayetaka kuhamia mjini... Hata kama mahari atatoa mume lakini hii ndiyo ndoa yenye ukakasi zaidi. Huvunjika mara tu wanapoanza kuishi wote mjini kama Wazazi au wahusika wasipokuwa makini.
Salama ya hii ndoa ni kuhama kutoka Mjini kwenda Kijijini.```
6.NDOA YA MIMBA.
```Hii Hufungwa kwa sababu wanaoowana hawataki kuonekana makwao kuwa wamezaa nje ya ndoa au Wazazi wametishia kumloga mwanaume kwa kumpotezea Zakali yake na muolewaji mara nyingi huwa hampendi muoaji kwa dhati au himbambikia mimba pia. Muoaji hutumia mimba kama mtego wa kuingia ndoani. Hii huvunjika mtoto akizaliwa na kufikisha mwaka mmoja(1) tu maana vinasaba huwa vinakataa kushabihina!```
7.NDOA YA MALI!
(UTAJIRI)
```Muolewaji {Binti} miaka 18 au 28 Muoaji 65 au 70. Ndoa hii pia huitwa ndoa ya Babu na Mjukuu. Ndoa ya aina hii hudumu, kwa sababu mwenye kauli ni mwenye mali. Asilimia kubwa ya waume wa ndoa hizi hulea watoto wasio wao.(Wanagongewa kweli kweli)```
8.NDOA KWA SABABU.
```Hufungwa ili mradi muoaji au muolewaji aonekane tu kwa jamii kuwa naye kaoa au kaolewa. Huwa hazina utii wala upendo dhati. Ndoa ya aina hii ikifikisha miaka mitatu (3) hadi mitano(5) huwa hazivunjiki wahusika huishi kwa mazoea hata kama wote au mmoja wapo mhepukaji,na Mara nyingi hawa hawaachanagi na wapenzi Wao wa zamani.```
9.NDOA YA UPENDO.
```Ndoa hizi ziliishia mwaka 1978 kabla ya vita vya Kagera. Muoaji na muolewaji hawakuangalia vitu ila utu tu ambao uliwaunganisha na kutengeneza upendo wa kudumu. Hii ilidumu miaka yote. Kwa sasa zipo chache sana! ''''
10.NDOA KUCHUMA
```Ndoa hii hufungwa mradi muoaji au muolewaji akapate kitu au vitu fulani kutoka kwa upande mmojawapo. Hii hudumu miaka kadhaa kutegemeana na malengo ya muhusika. Wengine husubiri mpaka muhusika afe, lkn hujikuta wanakufa wao kwanza! (Wengi sehemu wameumbuka sana)```

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search