Wednesday, 13 September 2017

Huyu Hapa Mbunge Aliyetaka Wabunge Wanawake Kutoa Ushahidi wa Wanaume Waliotahiriwa Wanavyonogesha Tendo la Ndoa

Huyu Hapa Mbunge Aliyetaka  Wabunge Wanawake Kutoa Ushahidi wa Wanaume Waliotahiriwa  Wanavyonogesha Tendo la Ndoa
Mbunge wa Konde, Khatibu Saidi Haji (CUF) amezua vicheko bungeni baada ya kuuliza swali ambalo linalohoji tafiti zinaonyesha kwamba wanaume waliotahiriwa wanakuwa active zaidi na wananogesha zaidi yale mambo (mapenzi).

Mbunge Khatibu ameuliza swali hilo leo bungeni mjini Dodoma, ambapo spika Ndugai alipinga kuwa hilo sio swali “hilo nalifuta sio swali sio swali” amesema Spika Ndugai.

“Tafiti zinaonyesha kwamba wanaume waliotahiriwa wanakuwa active zaidi na wananogesha zaidi yale mambo, Je Mhe. Spika katika hali hiyo wabunge wanawake kupitia bunge hili mtoe kidogo ushahidi wa haya wanaume waliokuwa hawajatahiriwa waige mfano huo?

alihoji Mbunge Khatibu.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search