Monday, 18 September 2017

LIPUMBA:-NITAWAONDOA WABUNGE WA MAJIMBO IWAPO WATAACHA KUNISIKILIZA NA KISHA KUMSIKILIZA MAALIM SEIF

Jana Prof Lipumba alikuwa na sherehe ya kuwapokea wabunge wa viti maalumu katika ofisi za chama Buguruni.Mkusanyiko huo ulioruhisiwa na polisi ulihudhuriwa na wanachama wengi wa CUF wa upande wa Prof Lipimba.

Katika sherehe hiyo,Prof Lipumba amenukuliwa akisema "Sina nia ya kufukuza wabunge wa majimbo,lakini kama watakuwa na kiburi cha kumsikiliza Maalim Seif,basi wembe ni uleule."

Lipumba anasema ana vijana wake aliowafundisha siasa toka akiwa mwalimu Chuo Kikuu,akimtolea mfano mbunge wa Malindi-Zanzibar,Mh.Ally Salehe.

Prof.Lipumba anasema wabunge wa majimbo,wasimsikilize Maalim Seif,akiwaita kwenye kamati ya Maadili ya chama,wafike haraka na sio kumsikiliza Maalim Seif ambaye atawaponza na wao wapitiwe na wembe kama wa wale wabunge wa kuteuliwa ambao saizi wanajuta kwa kumsikiliza Maalim Seif,na sasa wameonja ubunge wa miaka miwili,huku wakiwa na madeni tele waliyokopa kwa kudhani watakaa bungeni miaka mitano.

Baadhi ya wabunge wa kuteuliwa,wamesema wanaingia kazini,ili kuhakikisha CUF kinarudi kuwa chama kikuu cha upinzani,na katika maeneo watakayokuwepo,hakutakuwa na CHADEMA wala chama kingine cha upinzani kuibuka.

Lipumba amewaasa wabunga hao kuwa watii kwa viongozi wa chama,na watambue ofisi yao ipo Buguruni na sio sehemu nyingine

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search