Saturday, 9 September 2017

MCHUNGAJI MSIGWA ASHANGAZWA NA UKIMYA WA VIONGOZI WA DINI KUHUSU TUKIO LA TUNDU LISSU KUPIGWA RISASI

Mbunge wa Iringa Mjini Peter Msigwa amesema anashangazwa na viongozi wa dini kukaa kimya juu ya kujeruhiwa kwa Tundu Lissu (Mbunge wa Singida Mashariki).

Msigwa ambaye yuko Nairobi na viongozi wengine wa Chadema, waliomsindikiza Lissu aliyepigwa risasi na watu ambao hawajafahamika akitokea bungeni ametuma kwenye Twitter kwamba anawashangaa viongozi wa dini kukaa kimya mpaka sasa.

‘’Inanishangaza kuona viongozi wa dini mpaka sasa wamekaa kimya juu ya kujeruhiwa kwa Lissu! Na mwenendo wa siasa za Tanzania!’’amesema Msigwa kwenye ujumbe wake wa Twitte

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search