Thursday, 21 September 2017

MKE AMUUA MUME KWA KUMCHINJA BAADA CHANZO KIKIWA NI SIMU YA MCHEPUKO HUKO TINDE MKOANI SHINYANGA

Image result for kamanda wa polisi shinyanga
Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga Simon Haule
****
Mwanamke aliyejulikana kwa jina la Zena Mohamed (28) msukuma amemuua mme wake Bakari Salehe (35) Mzaramo kwa kumchinja na kisu shingoni upande wa kushoto.

Tukio hilo limetokea jana saa mbili na nusu usiku Septemba 20,2017 katika kitongoji cha Malenge kijiji cha Jomu,kata ya Tinde,tarafa ya Itwangi,wilaya ya Shinyanga mkoani Shinyanga.

Inaelezwa kuwa wanandoa hao walikuwa wamegombana,ndipo mke akamsubiri mmewe alale na alipolala akamchoma kisu tumboni na shingoni.

“Baada ya kutekeleza tukio hilo,mwanamke huyo alifungua radio kwa sauti ya juu kisha kumfunga mlango kwa kufuli kisha kukimbilia Shinyanga Mjini ambapo kuna Mama yake mzazi,alipofika akamwambia mama kuwa amefanya mauaji,hali iliyomfanya mama atoe taarifa polisi na kufanikisha kukamatwa kwa mtuhumiwa”,mashuhuda wameiambia Malunde1 blog.

Kwa mujibu wa Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga,ACP Haule amesema tukio hilo limetokea wakati wanandoa hao walipokuwa wanapigana katika ugomvi uliotokea nyumbani kwao.

“Chanzo cha tukio hilo ni wivu wa mapenzi baada ya mke kupokea simu ya mume wake iliyokuwa ikiita na kisha kusikia sauti ya mwanamke mwingine na kuhisi kuwa ni hawala wa muwe wake,ndipo ugomvi ulipoanzia”,ameeleza Kamanda Haule.

Kamanda huyo wa polisi amesema wanamshikilia mtuhumiwa kwa mahojiano zaidi na ametoa wito kwa wananchi kujiepusha na kuachana na vitendo vya dhana ya wivu wa kufikirika.

“Tuache kufikiri kuwa mwanaume akiongea na mwanamke au mwanamke akiongea na mwanaume kwa njia ya simu au njia ya kawaida lazima kuna mahusiano ya kimapenzi,jambo ambalo siyo kweli hasa kutokana na masuala ya utandawazi katika dunia hii ya leo”,ameeleza Kamanda Haule.

Imeandaliwa na Kadama Malunde-Malunde1 blog

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only

Start typing and press Enter to search